Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa Hilali Nyekundu ya Iran Mohammad Nasiri amesema kufuatia mlipuko huo wa Beirut, Hilali Nyekundu ya Iran inatuma misaada yenye uzito wa tani tisa. Aidha amesema Hilali Nyekundu ya Iran itafungua hospitali ya muda na kutuma timu ya madaktari na wahudumu wa afya 22 Lebanon katika awamu ya kwanza. Amesema misaada hiyo inatumwa kufuatia ombi la mkuu wa Hilali Nyekundu ya Lebanon George Kataneh.
Idadi ya watu waliouawa kwenye mripuko mkubwa katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, imepindukia 100, huku wengine 4,000 wakiwa wamejeruhiwa. Bado haijafahamika kilichosababisha mripuko huo, hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lebanon, Mohammed Fahmi, amesema huenda shehena kubwa ya kemikali ya ammonium nitrate kwenye bandari ya Beirut iliripuka.
342/